Nkurumah Street PO BOX 543 MWANZA Tel: +255 282500733 Fax: +255 282541484 Email:mwanza@tfda.or.tz

TFDA kanda ya ziwa yasimamia zoezi la uteketezaji wa bidhaa za dawa za Serikali zilizokwisha muda wake.

TFDA Ofisi ya Kanda ya Ziwa ilisimamia zoezi la uteketezaji wa bidhaa za dawa na vifaa tiba katika Manispaa ya Bukoba, na Halmashauri ya Wilaya ya Karagwe.
Zeozi hilo lilifanyika tarehe 30/09/213 hadi tarehe 03/10/2013.Dawa zenye uzito wa Tani 1.6 thamani ya TZS19,698,855/-.mali ya Hospitali ya Mkoa wa Kagera,. uzito wa Tani 3.15.na thamani TZS93,118,589.05/-Mali ya Halmashauri ya Wilaya Bukoba na uzito wa Tani 6.0 na thamani TZS65,629,010/- Mali ya Halmashauri ya wilaya ya Karagwe zilizokwisha muda wa matumizi ambazo zimekusanywa kwa kipindi kirefu sana zaidi ya miaka kumi ziliteketezwa.




Pichani  ni bidhaa za dawa na vifaa tiba zikiwa zinaandaliwa  kuwekwa katika INCENERATOR kwa ajili ya kuteketezwa
 
                                            .




Pichani ni bidhaa za dawa ambazo tayari zimeshaandaliwa kwa ajili ya kufukiwa katika ardhi.Dawa husika huchanganwa na chokaa na cement na kufanyika udongo mgumu tayari kufukiwa.


Pichani ni bidhaa za dawa ambazo zimetengwa na kufunganshwa tayari kwa kuchomwa.









Pichani ni Kikao cha Kamati ya kuteketeza bidhaa iliyoundwa na Mfamasia wa Mkoa,Mganga Mkuu wa Mkoa, Mhakiki Mali wa Mkoa, Afisa Usalama wa Taifa, Afisa wa Polisi, Mhakiki Mali kutoka Wizara ya fedha, Mwakilishi wa Mfamasia Mkuu wa Serikali , Mkaguzi wa Dawa Ofisi ya Kanda, TFDA, Afisa Afya wa Mkoa na wajumbe kutoka kwa Wafadhili (John Snow Inc)


TFDA kanda ya ziwa yateketeza bidhaa zisizokidhi viwango vya ubora

TFDA ofisi ya Kanda ya Ziwa imeteketeza bidhaa za vipodozi,dawa,vifaa tiba na chakula visivyokidhi vigezo vya ubora baada ya kukamatwa katika soko katika ukaguzi wa dawa uliofanyika tarere 11-19 mwezi julai 2013, ukaguzi wa vipodozi uliofanyika tarehe 22-29 mwezi Julai 2013 na ukaguzi wa kawaida kwa mwezi August.
Jumla ya bidhaa zenye uzito wa Tani 3.5 na thamani ya TZS 26,647,550 ziliteketezwa katika dampo la Jiji lililoko Buhongwa katika Manispaa ya Nyamagana.

watumishi wa Ofisi ya Kanda ya Ziwa wakiwa wanajiandaa na maandamano ya siku ya wafanyakazi







Pichani Wafanyakazi wa ofisi ya Kanda ya Ziwa wakiwa mbele ya ofisi ya kanda wanajiandaa kwenda kwenye maandamano ya Siku ya wafanyakazi Mei Mosi mwaka 2013

uteketezaji wa bidhaa kwa hiari


Wadau wanaojihusiha na biasahara ya bidhaa za chakula,dawa ,vifaa tiba na vipodozi wanapaswa kusalimisha kwa hiari bidhaa ambaza  hazifai kwa matumizi ,zilizokwisha muda wake na ambazo zimepungua ubora zikiwa sokoni ili kuweza kuteketezwa.
Pichani ni bidhaa za dawa na vifaa tiba za duka mojawapo la dawa Mwanza mjini zikiwa zinateketezwa chini ya usimamizi wa TFDA, TRA, Polisi n.k

Watumishi wa TFDA ofisi ya Kanda ya Ziwa ,wakiwa katika sherehe za siku ya wafanyakazi(Mei Mosi) Katika uwanja wa CCM Kirumba.


Pichani watumishi wa ofisi ya Kanda ya Ziwa,TFDA.wakiwa katika uwanja wa CCM Kirumba katika Sikukukuu ya wafanyakazi ya Mei Mosi


Shehena ya vipodozi vyenye viambata vya sumu vikiwa vinataka kusafirishwa kwenda Dar es salaam


Vipodozi vyenye viambata vya sumu vikiwa katika lori tayari kusafirishwa kwenda Dar es salaam. Vipodozi hivyo vilikamatwa na wakaguzi kufuatia msako mkali unaoendelea wa kukamata bidhaa zote za chakula,Dawa ,Vipodozi na Vifaa tiba ambazo hazijakidhi matakwa ya Sheria ya Chakula ,Dawa na Vipodozi namba 1 ya Mwaka 2003.

SHEHENA YA VIPODOZI VILIVYOPIGWA MARUFUKU KUTOKA NJE YA NCHI VIMEKAMATWA JIJINI MWANZA



Mkaguzi wa Dawa wa Ofisi ya Kanda ya Ziwa akiwa anaorodhesha bidhaa za vipodozi vilivyopigwa marufuku kufuatia kukamatwa kwa gari ambalo lilikua lina mzigo huo ukiwa umeingia nchini. Shehena hiyo ya vipodozi hivyo ilikua inaandaliwa kusafirishwa kwenda Jijini Dar es salaam.
Vipodozi vyote vilikamatwa na wakaguzi na zoezi la uteketezaji linaandaliwa kufanyika katika Dampo ya Buhongwa tarehe 24 Aprili 2013

OFISI YA MAMLAKA YA CHAKULA NA DAWA-MWANZA

Ofisi ya Kanda ya Ziwa ya Mamlaka ya Chakula na Dawa,TFDA iliyoko katika mtaa wa Nkurumah karibu na Benki ya Azania , Manispaa ya Nyamagana, Mkoa wa Mwanza

MFANYABIASHARA ANAYEUSISHWA NA UTENGENEZAJI WA LEBO ZA DAWA NA KUTUMIKA KATIKA MAKOPO YA DAWA


Pichani ni Mfanyabiashara mmoja aliye chini ya ulinzi (pingu mkononi)  kwa vile ‘Stationery’ yake ambayo aliuziwa na mfanyabiashara mwingine ilihusishwa na vitendo vya kutengeneza lebo za dawa na kutumika katika makopo ya dawa. Mtuhumiwa huyu alitoa taarifa zilizoweza kusaidia wakaguzi kupata alikohamia  muhusika. 

TFDA IKITOA ELIMU KWA UMMA KUHUSIANA NA SHUGHULI INAZOZIFANYA

Ofisi ya kanda ya Ziwa ikiwa katika moja ya maonyesho ikitoa elimu kwa uma kuhusiana na shughuli inazozifanya katika uthibiti wa usalama na ubora wa bidhaa inazozidhibiti zinazokuwepo katika soko la Tanzania.

TAARIFA KWA UMMA KUHUSIANA NA OPERESHENI YA DAWA DUNI/BANDIA

Ofisi ya Kanda ya Ziwa ya Mamlaka ya chakula na Dawa imekua ikipata ushirikiano mzuri sana na jeshi la polisi katika kutekeleza majukumu yake,
Pichani ni Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya chakula na Dawa na pembeni yake ni Aliyekuwa kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza Hayati Liberatus Baro wakiwa katika shughuli ya kutoa taarifa kwa umma kuhusiana na operesheni ya dawa duni/Bandia iliyofanika katika Mkoa wa Mwanza mwezi Juni mwaka 2012.kufuatia zoezi hilo kesi 7 zilifunguliwa na watuhumiwa 13 walifikishwa mahakamani.

MKURUGENZI MKUU WA TFDA AKITOA SEMINA KWA WAANDISHI WA HABARI

Ofisi ya Kanda ya Ziwa katika kutekeleza mpango kazi wake wa mwaka 2011/2012 iliandaa semina ya waandishi wa habari kutoka katika vyombo vya habari mbalimbali katika Mikoa ya Kanda ya Ziwa, ili kuweza kuwaongezea wana habari uelewa mpana kabisa katika kufahamu shughuli  za Mamlaka

Pichani ni Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya chakula na Dawa ,TFDA aliyesimama na pembeni yake ni Mkururgenzi wa Dawa na Vipidozi, DMC akiwa anatoa maelezo ya utangulizi katika kufungua semina hiyo  iliyofanyika katika ukumbi wa Nyakahoja,Manispaa ya Nyamagana Mwezi Julai Mwaka 2012

SEMINA KWA WAANDISHI WA HABARI

Pichani ni baadhi ya waandishi wa habari wakina wameshafika katika ukumbi wa Nyakahoja ulioko Mwanza Mjini tayari kwa semina hiyo.

UTEKETEZAJI WA BIDHAA


Ofisi ya Kanda ya Ziwa imekua ikiteketeza  bidhaa za chakula, dawa, vipodozi na vifaa tiba zisizofaa inazozikamata katika soko, pichani ni mazoezi tofauti ya uteketezaji wa bidhaa za chakula na dawa maliyofanyika katika dampo la Jiji lililoko Buhongwa

TFDA KANDA YA ZIWA IKISHIRIKIANA NA WAJUMBE WENGINE KAMA TRA,UHAMIAJI NA POLISI

Ofisi ya Kanda ya Ziwa ikishirikiana na wajumbe wengine kutoka katika ofisi mbalimbali kama TRA, Uhamiaji, Polisi n.k watakaotumia ofisi mpya zinazojengwa katika kituo cha mpakani  Mtukula  kama  ‘One stop boader post (OSBP) wakiwa katika ukaguzi wa maendeleo ya  ujenzi  wa ofisi hizo ambapo mkandarasi aliahidi kuwa ifikapo mwezi April mwaka 2013 atakua amemaliza kazi.

VIPODOZI VYENYE VIAMBATA VYA SUMU

Bidhaa za vipodozi vyenye viambata vya sumu vikiwa vimekamatwa kutoka katika ghala la mfanyabishara vikiwa vimetoka kushusha kwa roli kutokea nchi jirani ya Kenya.Vipodozi hivi vilikamatwa na kesi ilifunguliwa

UKIUKWAJI WA UENDESHAJI WA BIASHARA YA DAWA


Ukiukwaji wa uendeshaji wa biashara ya dawa kiasi ambacho huduma za matibabu hutolewa katika maduka ya dawa ulipelekea mpango wa maduka ya dawa muhimu ambapo zaidi ya kwamba maduka haya kisheria yataweza kuuza baadhi ya dawa za cheti lakini pia watoa dawa watasoma na kuelewa umuhimu wa kufuata taratibu katika kuendesha biashara ya duka la dawa ambapo vitendo kama hivi katika picha vitatokomea kabisa.
Pichani ni duka moja Mkoani Kagera wilayani Karagwe likiwa na vifaa tiba vitendanishi na pia sindano iliyotoka kutumika kwa mgonjwa pembeni yake ilikutwa chupa ya penadur ikiwa imetoka kutumika.Duka husika lilifungwa.

KIWANDA KIKIPAKA RANGI KUTA,UZALISHAJI UKIENDELEA


Kiwanda kimoja cha Biscuits Mwanza Mjini kilikutwa kinapaka rangi baadhi ya kuta zake eneo la uzalishaji wakati shughuli za uzalishaji wa biskuti zikiwa zinaendelea.Kiwanda husika kilifungwa na kutakiwa kumaliza shughuli za kupaka rangi kabla uzalishaji haujaendelea.Pembeni ni makreti ya biskuits ambazo zilizuiliwa.

TAFRIJA YA KUAGWA KWA ALIYEKUWA MENEJA WA KANDA-TFDA





Tafrija ndogo ya chakula cha jioni iliyofanyika katika ukumbi wa hoteli ya JB Delmonte ya kumuaga aliyekua Meneja wa Ofisi ya Kanda ndugu Seth Kisenge na kumkaribisha Kaimu Meneja Mpya Ndugu Moses Mbambe

Powered by Blogger.